Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TID atoka kali, sijawahi kukutana na Alikiba, ‘Ni mwarabu eeeh?’

ALIKIBA NA TID TID atoka kali, sijawahi kukutana na Alikiba, ‘Ni mwarabu eeeh?’

Tue, 8 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaweza kuona ni masihala lakini ndivyo alivyo staa wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed ‘TID’ siku za hivi karibuni amekuwa akitoa vituko vya aina yake ambapo juzikati alitoa kipya baada ya kusema hajawahi kukutana na Alikiba, staa wa Bongo Fleva.

TID alitoa kioja hicho kwenye uzinduzi wa albamu ya Dimpoz inayokwenda kwa jina la Dedication ambapo mastaa mbalimbali wakubwa walihudhuriwa akiwemo Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.

“Dimpoz ni kijana wangu nimekuwa naye kwa takriban miaka mine tukiimba naye kwenye bendi yangu, anajua kujiongeza kama unavyoona kwenye albamu amewashirikisha wasanii kama Jux na yule dogo Marioo.

“Angalia amemshirikisha Alikiba, sijawahi kukutana naye mimi kabis. Me I think Alikiba is Arabian Alikiba ni mwarabu eeh,” alisema TID.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live