Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TID amshauri Kajala kuwa mtulivu

9f17b73cf53855f574c08679d6b51e96 TID amshauri Kajala kuwa mtulivu

Fri, 19 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Khalid Mohamed ‘TID’ amemshauri rafiki yake wa siku nyingi mwigizaji Kajala Masanja kuwa mtulivu kipindi hiki ambacho anakumbana na changamoto kwa mtoto wake Paula.

Hivi karibuni msanii Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny alivujisha video chafu kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha akimbusu mtoto wa Kajala, Paula tukio ambalo halikumfurahisha mzazi wa binti huyo na kuchukua hatua za kuripoti polisi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, TID alisema kwa vile kwa sasa suala hilo linashughulikiwa na mamlaka za kisheria, Kajala anapaswa kutulia na kuwa na amani ya roho.

“Kama mzazi namshauri Kajala awe mtulivu kwasababu kilichotokea ni stori yenye kuhuzunisha kwa mzazi, unajaribu kumlea mtoto wako vizuri kisha changamoto nyingine zinatokea

waache suala hilo kujua mamlaka zitafanyeje,” alisema.

Wahusika juzi waliitwa polisi kituo cha Osterbay na kuhojiwa suala hilo na uchunguzi unaendelea.

TID aliyewahi kuvuma na ngoma kadhaa ikiwamo Zeze, Unaniroga, Woman na nyingine kadhaa ni mmoja wa marafiki wa Kajala wa muda mrefu tangu kabla hata hajaanza kuimba muziki.

Chanzo: habarileo.co.tz