Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TID ajivunia kuitwa mnyama ‘ nimewa-inspire wengine kuitwa simba’

7405 Screen Shot 2018 05 03 At 10.09.58.png TZW

Fri, 4 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii mkongwe wa muziki, Khalid Mohamed aka (TID) amefunguka kuelezea namna alivyolipata jina la ‘mnyama’ ambalo amekuwa akilitumia kama aka ukiachana na jina lake ya TID.



Muimbaji huyo ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu, amedai jina hilo alilipata kutoka kwa mashabiki baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kuimba na kucheza kwa wakati mmoja.

“Kwa mfano mimi perfomance zangu wanasema ni kali, yaani za kinyama, kwahiyo mimi nilikuwa nafanya kinyama ndipo mashabiki walipo amua kunipa jina la mnyama, mpaka sasa mimi ni mnyama kutoka unyamani” TID alikiambia kipichi cha On The Street cha ETV.

Aliongeza, “Lakini sio mbaya sasa hivi nasikia kuna wengine wanajiita Simba, nimewa-inspire kuwa hivyo, kuna wengine ni wakufungwa, lakini ndio mnyama wenyewe,”

Muimbaji huyo kwa sasa anajipanga kuachia kolabo aliyoshirikishwa na msanii Slimm ambaye kwa sasa ameoneka kuwa karibu na muimbaji Davido wa Nigeria.

Loading...
Chanzo: bongo5.com