Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TID, P Diddy hawajaoa mpaka sasa

Tid Diddy TID, P Diddy hawajaoa mpaka sasa

Fri, 28 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Acha tukurudishe nyuma kidogo wakati Puff Daddy or P Diddy @diddy alipoachia ngoma ya 'I need a girl' kutoka Album ya 'We Invented The Remix' kwaka 2002.

#PDiddy alitaja sifa kibao za msichana anayemtaka wa kumfanya kuwa mke wake, aanzishe naye familia, awe wake wa maisha na kufa na kuzikana ila hajui yupi ana upendo wa kweli anaona wengine watamtumia tu sababu ya ustaa wake.

Mwaka mmoja baadaye Top In Dar @tidmusic akaibuka na ngoma ya 'Girlfriend' ambayo akiachia mpaka movie yake.

Picha linaanza #TID amepigika kinoma ila anatafuta mpenzi mwenye vigezo ambavyo anavitaka mfano awe naye kwenye shida na balaa, awe na maringo kama ya Twiga, kucha za Kung'aa na pamba za kuvaa pia ampende na umaskini wake.

Ukisikiliza nyimbo zote hizo 'I need a girl' ya P Diddy na 'Girlfriend' ya TID ki-content zinafanana na wote wamezungumzia sifa na vigezo vya mpenzi/mke wanayemtaka.

Licha ya kutoa sifa na vigezo kwa wanawake wanaowataka lakini mpake leo Diddy na TID hawajaoa ila wamepitia mahusiano mbalimbali na wanawake tofauti tofauti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live