Hawa ni wasanii ambao walitengeneza maisha katika kipindi ambacho muziki haukuwa na pesa za kutosha, kidogo walichokipata walikitunza na kukiwekeza sasa hivi wanaishi maisha mazuri.
A.Y alitengeneza njia ya ya kimataifa kisha akawapa connection wadogo zake wakina mondi na kiba akawaachia kijiti wanatembea.
Professor Jay alishawishi vijana wengi kuingia kwenye muziki baada ya kuwaaminisha wazazi wengi kuwa muziki sio uhuni kwa kutoa nyimbo mbalimbali za kuelimisha na kupendwa na jamii nzima.
Mwana FA akatuaminisha kwamba unaweza kuwa msomi ukafanya muziki na bado ukabaki na heshima yako ukijitambua akaaminiwa na serikali sasa hivi ni waziri.
Hawa wote wamefanya kazi na wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa, wanaishi vizuri na wadogo zao na madogo nao wanawapa heshima ya kutosha, huwezi msikia Harmonize, alikiba au Diamond Platnumz akimsema vibaya yoyote kati ya hao wakongwe, wala huwezi kusikia hawa wakongwe wakiwasema vibaya wadogo zao.
Kuna wakati wasanii wakongwe ambao hawajajijenga kiuchumi wanakuwa na hasira na wadogo zao sababu ya stress za ufukara ambao wameutengeneza wenyewe kwa kushindwa kujiwekeza kwa kile walichokuwa wanakipata.
Tafuta msanii yeyote wa zamani mwenye pesa uone kama anagombana na vijana wasasa halafu angalia wale ambao hawana kitu wanavyo wachukia wasanii wa sasa.