Mwanamuziki maarufu kutokea Ireland Sinead O’Connor (56), amefariki dunia.
Msanii huyo alitamba sana katika miaka ya 1990 kwa kibao chake cha "Nothing Compares 2 u" ambacho kilimfanya kuwa nyota mkubwa duniani.
Kupitia mtandao wa X Waziri Mkuu wa Ireland, jana Varadkar ametuma salamu za rambirambi kwa familia na wapenzi wote wa muziki , na kuandika kuwa “ Muziki wake ulipendwa duniani kote na talanta yake haikuwa na mfano , haikuweza kulinganishwa”.
Sinead alibadili dini na kuwa Muislamu mwaka 2018 na kubadili jina lake kuwa Shuhada Sadaqat hata hivyo kisanii aliendelea kutumia jina lake la mwanzo.
Mwaka 2021 msanii huyo alifuta mipango yake yote ya kazi na kutangaza kuwa anachukua mwaka mmoja wa matibabu kutokana na msongo wa mawazo na matumizi ya dawa za kulevya yaliyokithiri.
Mtoto wake wa kiume Shane (17) alipotea mwaka jana na baadaye kukutwa akiwa amejiua. Jambo hili lilimpelekea msongo mzito wa mawazo na afya yake kutetereka.