Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANZIA: Mama mzazi wa Lady Jaydee afariki dunia

7101 15337232 1366499483369419 2194378132457259008 N TZW

Thu, 26 Apr 2018 Chanzo: bongo5.com

Mama mzazi wa msanii Lady Jaydee, Bi. Martha Mbibo amefariki dunia.



Bi. Mbibo amefariki alfajiri ya leo Aprili 26, 2018 akiwa nyumbani kwake Jet, Dar es Salaam.

Akithibitisha taarifa hizo kaka wa Lady Jaydee ambaye pia ni msanii Dabo, amesema mama yao amefariki mara baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.

April 01, 2018 Lady Jaydee alizungumza kuhusu kuugua kwa mama yake mzazi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika;

Nauguza mama mzazi lakini naendelea kupambana na maisha vilevile, usinione naimba au natabasamu ukafikiri nina raha sana.

Sina raha wala nini, lakini pia lazima nifanye kazi ili niweze kuishi, bila kuangalia kama watu watani judge vipi!, Kwani bado naamini Mungu atamponya na kumnyanyua kwenye kitanda alicholala kwa zaidi ya miezi 2, Kwani Mungu pekee ndio anaeweza.

Bi. Mbibo alianza kuugua tangu mwishoni mwa mwaka 2016 ambapo alipatiwa matibabu hapa nchini na nje ya nchini (India).

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Jet, Dar es Salaam, na familia itatoa utaratibu wa mazishi mara baada ya utaratibu wa kuupeleka mwili hospitali kuhifadhiwa kukamilika.

Endelea kuwa karibu na Bongo5 kwa taarifa zaidi za msiba huo.
Chanzo: bongo5.com