Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANZIA: Dj Steve B wa Clouds FM afariki Dunia

DJ Steve B Steven Mdoe maarufu kama DJ Steve B

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa DJ wa CloudsFM Steven Mdoe maarufu kama DJ Steve B amefariki dunia jana Julai 31 Hospitalini Jijini Dar es salaam huku chanzo kikitajwa kuwa ni kupanda kwa presha.

Amstrong Mdoe ambaye ni Kaka wa Marehemu amesema kuwa Steve B ambaye alikuwa akisumbuliwa na figo toka mwaka 2019 alipelekwa Hospitali juzi na kuwekwa ICU baada ya presha kupanda na baadaye kupanda zaidi na kumsababishia kupoteza fahamu kwa siku tatu kabla ya kufariki.

"Steve B alipoteza fahamu kwa siku 3 ambapo jioni ya Julai 31 saa 10 akafariki, alikuwa na tatizo la figo kwa miaka minne tangu 2019 lakini figo sio chanzo cha kifo chake, taratibu za mazishi bado tunazungumza tupange utaratibu lakini tunapokea rambirambi kwa namba 0678689383"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live