Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANZIA: Bongo Movie yapata pigo zito

MZEE KORONGO KUFA.jpeg Mzee Korongo

Mon, 22 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji mkongwe wa Bongo Movies, Hamisi Korongo maarufu kama Mzee Korongo amefariki dunia leo Jumatatu, Agosti 22, 2022 katika Hospitali ya Mwananyamara jijini Dar es Salaam.

Taarifa za awali zinadai kuwa Mzee Korongo alilazwa hospitalini hapo akipatiwa matibabu siku chache kabla ya umauti kumkuta.

Taarifa hiyo imetolewa na moja ya msanii mashuhuri Susan Lewis maarufu kama Natasha Mamvi, kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa ameposti picha ya marehemu ilioambatana na ujumbe huu;

“Mzee Hamisi Korongo tulijitahidi lakini mungu amekupenda zaidi, pumzika kwa Amani’” ameandika Natasha Mamvi.

Miongoni mwa filamu alizowahi kucheza na zikatikisa ni ile ya Siri ya Giningi, Tego la Kijiji, Suluhu, Ghadhabu na nyingine nyingi.

Taarifa zaidi tutaendelea kukujuza endelea kuwa nasi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live