Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAMTHILIA YA SULTAN: Patrick Masele ndiye aliyeigiza sauti ya Mtukufu Sultan

Tue, 5 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ni tamthiliya inayohusu maisha ya Sultan Suleyman. Katika umri wa miaka 26 alianza mbio za kuitengeneza himaya yake ya Ottoman akitaka iwe kubwa kuliko ya Alexander the Great. Utawala wake wa miaka 46 ulihitajika ulimwenguni kote akiwa na Pargali Ibrahim.

Nafasi ya Mtukufu Suleiyman imechezwa na Halit Ergenc aliyezaliwa 1970 ni mwigizaji maarufu nchini Uturuki.

Halit ameshacheza filamu mbalimbali ikiwemo Binbir Gece ya mwaka 2006 na Dersimiz: Ataturk iliyotoka mwaka 2010 kabla ya kuanza kuonekana kwenye tamthilia ya Sultan.

Pamoja na kwamba kielimu ni mhandisi wa vyombo vya majini, lakini amejaliwa vipaji vingine mbali ya kuigiza ni mwitikiaji mzuri wa nyimbo za wasanii ’backing vocalist’ na mcheza shoo wa waimbaji.

Patrick Masele

Patrick alijikuta akifanya kazi hiyo baada ya Azam kutafuta watu ambao wameshawahi kufanya kazi hizo.

Alikuwa mmoja wao ambao walikuwa wakifanya kazi na Shirika la Media For Development International ambao ndio walitengeneza tamthilia ya Siri ya Mtungi na Wahapahapa.

Pia, ndio waliotengeneza katuni ya kirukuu iliyojizolea umaarufu mkubwa miaka mitatu iliyopita. Katika katuni hiyo, Patrick anasema alicheza kama babu wa Kirukuu na kaigiza sauti kama Mzee wa Mlimani .

Katika maelezo yake anasema ameshacheza matangazo mbalimbali yakiwemo ya vinywaji wakati kwenye kuingiza sauti ana ujuzi wa zaidi ya miaka mitano.

Anasema kutokana na uzoefu huo kwake haikumuwia vigumu katika kuigiza sauti ya Sultan na pia ameweza kuwa mwalimu wa wengine katika fani hiyo.

Hata hivyo, anasema baada ya watu kumjua yeye ndiye anaigiza sauti ya Sultan, amekuwa akipata shida mtaani ikiwemo kumlaumu kwa maamuzi ambayo amekuwa akiyachukua dhidi ya watu mbalimbali.

Je ameisomea kazi ya kuingiza sauti?

Patrick anasema kazi hiyo hajaisomea ila amekuwa akijifunza kupitia mitandao.

Hata hivyo, anasema kutokana na kuonekana kuwa na uhitaji kwa sasa, ipo haja ya vyuo vinavyofundisha sanaa kujiongeza.

Akitolea mfano wanachokifanya Azam kuwa na tamthilia zilizotafsiriwa Kiswahili zisizopungua nne, zimeweza kuajiri vijana zaidi ya 50.

Hivyo anasema ni njia nyingine ya watu kujipatia ajira, ukizingatia utawala wa awamu hii ya tano unasisitiza watu kufanya kazi.

Anabainisha kwamba wahusika wataweza kufanya vizuri zaidi endapo watakuwa wamesomea kazi hiyo na huenda mwisho wa siku wakafungua na ofisi zao.



Chanzo: mwananchi.co.tz