Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAMTHILIA YA SULTAN: Mjue Salma Salim anaigiza sauti ya Monica Gritti

38742 SULTANI+PIC TAMTHILIA YA SULTAN: Mjue Salma Salim anaigiza sauti ya Monica Gritti

Tue, 29 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kuhusu Monica Gritti

Katika tamthilia hii Monica Gritti, ambaye ni dada wa Signore Gritti, alifika katika kasri la mfalme kwa lengo la kumsalimia kaka yake huyo.

Nafasi hii imechezwa na Berguzar Korel. Muigizaji wa Uturuki aliyeanza kucheza filamu akiwa anasoma chuo cha sanaa. Filamu alizowahi kucheza ni pamoja na “1001 Nights”, “Karadayi”, “Kurtlar Vadisi Irak” na “Wounded Love.

Salma Salim

Salma ndiye ameigiza sauti, mbali na Monica pia ameigiza sauti za masuria wengine.

Kwa msiofahamu, masuria ni wasichana ambao hununuliwa utumwani kwa lengo la kwenda kutumikishwa katika himaya ya mfalme kama watu wa kumburudisha.

Lakini wakipata nafasi ya kuingia katika chumba cha mfalme na kupata mimba wana nafasi kubwa ya kupandishwa vyeo.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Hurrem na Mahidevran kabla hawajawa wake wa mfalme Sultan.

Salma kitaaluma ni muigizaji na mwanamuziki. Anasema malengo yake ni makubwa, ikiwemo kuja kuwa msanii mkubwa na kuitangaza Tanzania kama ilivyo kwa wasanii wengine waliotangulia.

Hata hivyo anasema watoto wa kike wanakabiliana na changamoto nyingi ikiwemo kuombwa rushwa ya ngono.

Pamoja na yote hayo, Salma anasema katika hili msichana pia unapaswa kuwa makini na kujua nini unachotaka na kuongeza kuwa wengi wanakwama hasa pale wanapotaka kurekodi ambapo kama kipato ni kidogo prodyuza ndio hapo anaingiza mambo yake na kama ni mwepesi unaingia kwenye 18 zake.

Anasema pamoja na changamoto hizo anashukuru yeye ameweza kutengeneza nyimbo tatu hadi sasa huku akiwaomba mashabiki kumpokea katika soko hilo la muziki.



Chanzo: mwananchi.co.tz