Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAMTHILIA YA SULTAN: Mfahamu aliyeigiza nafasi ya Hurrem Sultana

61419 Pic+huren

Thu, 6 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hakuna ubishi kuwa watizamaji wa king’amuzi cha Azam , hawakai mbali na runinga zao inapofika saa nne kamili usiku.

Hukaa pembeni ya runinga zao kutizama tamthilia inayovutia wengi iitwayo Sultan.

Tamthilia hii mbali na kuigizwa kwa maudhui ya kifalme imevutia wengi kutokana na kuwapo kwa mchuano mkali kati ya Sultan na wakeze mmoja wao Hurrem ambaye alifariki jana katika mwendezo wa tamthilia hiyo.

Mke wa Sultan Suleiman, Hurrem anayevutia wengi kutokana na kuicheza vyema nafasi yake ni Hurrem Sultana au Meryem Sarah Uzerli kama alivyoandikishwa na wazazi wake katika cheti cha kuzaliwa.

Hurrem ni nani?

Hurrem ni mwigizaji aliyezaliwa mwaka 1983 ana asili ya Uturuki na Ujerumani, aliibuka kuwa maarufu kupitia filamu ya Kituruki iitwayo Sultan iliyoigizwa mwaka 2011 hadi 2013 ambayo ni maarufu hadi leo na imeshinda tupz nyingi ikiwamo ya heshima ya nchini humo Golden Butterfly.

Pia Soma

Mtunzi wa filamu hiyo Meral Okay alitafuta mwigizaji atakayemudu nafasi hiyo kwa miezi minne kabla ya kumchagua Hurrem.

Ameiigiza vema nafasi ya Hurrem aliyewahi kuishi karne ya 21 na alikuwa ni mke wa Sultan Suleima.

 

Kwa nini ni kivutio?

Hurrem aliigiza nafasi ya mwanamke aliyekuwa mke wa mfalme Suleiman aliyewahi kuishi karne ya 16.

Mfalme Suleiman wa Ottoman ambaye ufalme wake ulikuwa na nguvu na aliitawala Ulaya, Asia na Afrika, akipanda kiti cha enzi katika Palace ya Topkapi wakati alikuwa na umri wa miaka ishirini na sita tu.

 

Licha ya kuwa na utawala wenye nguvu alikuwa anapenda wanawake na hata watumwa akiwamo Hurrem Sultana ambaye alikuwa ni mtumwa kutoka Ukrain na kuishi katika jumba la kifalme Stanbury nchini Uturuki.

 

Hurrem alibadili maisha ya Halem ya Sultan Suleiman kwa kuipinga tabia ya Sultan kutamani wanawake kwa kuanzisha vita na kila anayechukua nafasi yake.

 

Ujio wake kwenye haremu (palace) akiwa ni mtumwa na kupewa jina la Hurrem lenye maana ya mwenye tabasamu zuri uliwafanya wake wa kwanza wa mfalme Sultan Gülfen na  Mahidevran kukosa nafasi ya kuwa karibu naye zaidi yake.

Baada ya miezi tisa alizaa mtoto wa kwanza wa kiume aliyepewa jina la Mehmed na kuwa na nafasi kama mama wa mfalme ajaye na kuendelea na kupata watoto sita akiwamo binti mmoja.

Mahidevran alimchukia Hurrem kiasi cha kumpangia njama za kila aina kwa sababu ya hofu ya kijana wake Mustafa ambaye alikuwa mkubwa kuliko watoto wa Hurrem kukosa nafasi ya ufalme, akiamini ushindani umeongezeka.

Maringo yake, anavyoshinda njama anazofanyiwa na sauti ya aliyetumika kuzungumza kwa lugha rahisi ya Kiswahili kumeifanya filamu hiyo kuwa kivutio.

Kuna mahali alikuwa anafanya vituko na ubabaifu wa wazi, mashitaka yakimfikia Sultan hukasirika na kumwita kwa ajili ya kumuonya, lakini akimuona hubadili mawazo na kuishia kumbusu.

Tukutane kwenye Sultan Suleiman tuone nini kinaendelea.

 

Hurrem wa kwanza aliondolewa baada ya kupata msongo wa mawazo

Mmoja wa waigizaji wakuu wa tamthilia hiyo Meryem Uzerli maarufu Hurrem alicheza katika msimu wa kwanza hadi wa tatu lakini katika ule wa nne ikachezwa na Vahide Perçin.

Mtayarishaji wa tamthilia hiyo, TImur Savci alisema Meryem aligua ugonjwa ‘burnout syndrome’ unaosababishwa na mtu kukinai jambo Fulani na hivyo kushindwa kuendelea kulifanya.

Hata hivyo, zilikuwa tetesi kwamba walishindwana katika malipo na hivyo mwanamke huyo akaamua kutimkia Ujerumani ambako mmoja wa wazazi wake wanatokea.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz