Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAMTHILIA YA SULTAN: Mfahamu Yvonne Cherly 'Monalisa' anayeigiza kwa Kiswahili sauti ya Hurreim Sultan

36729 Pic+monalisa TAMTHILIA YA SULTAN: Mfahamu Yvonne Cherly 'Monalisa' anayeigiza kwa Kiswahili sauti ya Hurreim Sult

Wed, 16 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kuhusu Hurreim

Hurreim Sultan ni mke wa Sultan Suleyman ambaye kajaliwa kuzaa naye watoto watano huku akionekana kuwa mwanamke mwenye msimamo na anayeogopewa na watu katika himaya hiyo ya Ottoman.

Nafasi hii imechezwa na watu wawili akiwemo Meryem Uzerli na Vahide Percin ambaye ndiyo anaonekana kwa sasa.

Vahide Percin ni mzaliwa wa Uturuki huku baba yake akiwa dereva wa malori na mama yake akiwa mama wa nyumbani.

Pamoja na kupitia elimu mbalimbali pia Vahide amesomea sanaa katika Chuo Kikuu cha Dokuz Eylul.

Akiwa na umri wa miaka 26, Sultan Suleyman alianza mbio za kuitengeneza himaya yake ya Ottoman akitaka iwe kubwa kuliko ya Alexander the Great.Utawala wake wa miaka 46 ulihitajika ulimwenguni kote akiwa na Pargali Ibrahim.

Kuhusu Hurreim

Hurreim Sultan ni mke wa Sultan Suleyman ambaye kajaliwa kuzaa naye watoto watano huku akionekana kuwa mwanamke mwenye msimamo na anayeogopewa na watu katika himaya hiyo ya Ottoman.

Nafasi hii imechezwa na watu wawili akiwemo Meryem Uzerli na Vahide Percin ambaye ndiyo anaonekana kwa sasa.

Vahide Percin ni mzaliwa wa Uturuki huku baba yake akiwa dereva wa malori na mama yake akiwa mama wa nyumbani.

Pamoja na kupitia elimu mbalimbali pia Vahide amesomea sanaa katika Chuo Kikuu cha Dokuz Eylul.

Yvonne Cherly ‘Monalisa’

Kwa hapa Bongo sauti hii imenakilishwa na muigizaji maarufu nchini Yvonne Cherly maarufu kwa jina la ‘Monalisa’.

Monalisa anasema pamoja na kwamba kazi hiyo si ngeni kwake lakini yapo aliyojifunza kupitia tamthilia hiyo ambayo inaonekana bora na kupendwa na watu.

Anasema mojawapo ni suala zima la vifaa, kwani Waturuki wameonekana kuwa vizuri katika vifaa vya kuchukua picha.

Jingine anasema bajeti yao ni kubwa na hivyo kusaidia kutengeneza filamu ya kueleweka, kwani pamoja na watu kuwa wengi katika tamthilia hiyo lakini kila mmoja kaweza kuvaa mavazi yanayohitajika katika sehemu husika.

Anasema anatamani hata yeye siku moja wawekezaji hapa nchi wawekeze kwa kiwango hicho ili Tanzania nayo iwe na kazi zinazoweza kuuzika kimataifa kama ilivyo kwa Sultan.

Katika tasnia ya filamu, Monalisa ameshapata tuzo mbalimbali ikiwemo muigizaji bora wa kike katika tuzo za Taffa mwaka 2015, muigizaji bora wa kike katika tamasha la Zifff mwaka Ziff 2010.

na mwaka jana alipata tuzo ya muigizaji mwenye ushwaishi Afrika na kuonekana kuwa ndoto ya wasichana wengi wanaotaka au kuingia kwenye tasnia hiyo

Chanzo: mwananchi.co.tz