Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAMTHILIA YA SULTAN: Magreth Semhando ndiye aliyeigiza sauti ya Rumeysa Hatun

38232 Sultan+pic TAMTHILIA YA SULTAN: Magreth Semhando ndiye aliyeigiza sauti ya Rumeysa Hatun

Fri, 25 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kuhusu Rumeysa Hatun

Rumeysa Hatun, binti aliyekuwa bila familia yake na kujikuta anaangukia kwenye mikono ya familia ya Sehzade Mustafa.

Akiwa hatamani hata kidogo kutoka katika familia hiyo, anajitokeza dada yake aitwaye Sinyora na kumueleza kuwa ana nia ya kumrudisha kwenye familia yao halisi jambo ambalo mrembo huyo hakubaliani nalo.

Ili kuhakikisha mbinu zake hizo zinafanikiwa, Rumeysa ameanza harakati za kumtega kimapenzi kulazimisha kuingia kwenye kundi la masuria ili amvutie.

Nafasi hii imechezwa na watu wawili ambao ni Elif Atakan na Busra Ayayd?n. ni muigizaji maarufu nchini Uturuki, ameshacheza filamu mbalimbali ikiwemo Ruya na En iyi arkadasim.

Magreth Semhando

Nafasi hii imeigizwa sauti na Magreth ambaye anasema kupitia mhusika wake, jamii inafundishwa kuwa na tabia ya kupambana kupata kile unachokitaka lakini si kwa njia zisizo halali.

Akimtolea mfano Rumeysa, anasema wakati majina ya masuria yakiitwa kwenda kumburudisha sultan yeye hakuwepo lakini alijipenyeza na kupita na tayari Schezard ameonyesha kuanza kuvutiwa naye.

Mbali ya kunakilisha sauti, Magreth anasema yeye ni mfanyabiashara anayeuza juisi na pia amesoma elimu ya biashara katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

“Nashukuru kwa kipaji hiki cha kunakilisha sauti kwani kinaniwezesha kuendesha maisha yangu ya kila siku ikiwemo kuongeza mtaji katika biashara zangu,” anasema Magreth.



Chanzo: mwananchi.co.tz