Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAMTHILIA YA SULTAN: Frank Samatwa mcheza ngoma anaemwakilisha Mustafa Pasha

Fri, 4 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Akiwa na umri wa miaka 26, Sultan Suleyman alianza mbio za kuitengeneza himaya yake ya Ottoman akitaka iwe kubwa kuliko ya Alexander the Great.Utawala wake wa miaka 46 ulihitajika ulimwenguni kote akiwa na Pargali Ibrahim.

Kuhusu Mustafa Pasha

Huyu ni Mkuu wa Jeshi nafasi hii imechezwa na Murat Sahan.Ni mwigizaji aliyewahi kucheza filamu ya Resurrection: Ertugrul (2014), Ver Kac (2017) na Magnificent Century (2011).

Frank Samatwa

Msanii huyu ananakilisha sauti za watu wawili akiwemo Mustafa Pasha na Yahaya Efend.

Mbali ya kunakilisha sauti, Samatwa ni msanii wa sanaa za majukwaani na mcheza ngoma za asili.

Kuhusu kazi ya kunakilisha sauti anasema kinachotakiwa ni kuwa na uwezo wa kucheza sauti mbalimbali ikiwemo ya mzee, kijana, mtoto ambazo hizi ukizimudu ni rahisi kunakilisha.

Uwezo huo anasema ndio umempa fursa ya kuigiza sauti za watu wawili tofauti katika tamthiliya hiyo.

Anasema moja ya kazi anayopenda kuifanya mbali na hiyo ni kuwa karibu na watoto na kuwafundisha kazi za sanaa anazofanya.

Wito wake kwa vijana anasema wafanye kazi badala ya kukaa na kuishia kulalamika kuwa maisha magumu.



Chanzo: mwananchi.co.tz