Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAMTHILIA YA SULTAN: Bakari Khalid mwandishi wa Habari anayeigiza sauti ya Lufti Pasha

35262 Pic+sultan Lufti Pasha

Wed, 9 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kuhusu Lufti Pasha

Lufti Pasha kwenye tamthilia hii mbali ya kuwa Waziri Mkuu wa sasa wa Ottoman, pia ni mume wa Sah Sultan na baba mzazi wa Esmehan.

Nafasi hii imechezwa na Mehmet Ozgur.Muigizaji huyu alijizolea umaarufu pale alipocheza filamu ya Tepenin Ardi na ile ya Game of Silence zilizotoka mwaka 2012 na Sari sicak ya mwaka 2017.

Bakari Khalid

Anayenakilisha sauti ya Lufti Pasha ni Bakari Khalid. Huyu kitaaluma ni mwandishi wa habari na alishafanya kazi vituo mbalimbali ikiwemo Azam na redio nyinginezo.

Katika tamthilia hii Bakari ananakilisha sauti ya Lufti Pasha ambaye anaeleza kuwa anampenda kwa kuwa ndiye anayemfanya ewe katika kazi hiyo ya kunakilisha kwa sasa.

Moja ya sifa yake kuu inayomvutia anasema ni mtu ambaye anapenda kumnyenyekea mkubwa wake na anapenda uongozi japokuwa hajui hapo baadaye atakuwaje.

Kuhusu malengo yake 2019, msanii huyu anabainisha kuwa anatamani kujifunza kupitia waandishi wa habari wakongwe akiwemo Charles Hillary, Salum Kikeke, Baruani Muhuza na ikiwezekana kuwapita.

‘Pia mwanadamu yeyote hutamani kupata kazi nzuri inayomnufaisha kama kijana.

‘Hivyo kwangu ndani ya mwaka huu mpya wa 2019 ni kuendelea kuchapa kazi ili yale ambayo sikuyafikia mwaka 2018 niyafanikishe,” anasema Bakari.



Chanzo: mwananchi.co.tz