Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAMTHILIA YA SULTAN; Aisha Ngoma anayeigiza sauti ya Hatice Sultan

Wed, 26 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kuhusu Hatice Sultan

Jina lake halisi ni Selma Ergec. Ni msichana mwenye uraia wa Uturuki na Ujerumani. Mbali ya kuwa mwigizaji pia amewahi kushiriki mashindano ya urembo lakini kwa sasa anajishughulisha na kazi za ubunifu na uanamitindo zaidi.

Aisha Ngoma

Kwa Tanzania Aisha Ngoma ndiye anayeigiza sauti ya Hatice Sultan.

Mbali ya kunakilisha sauti pia ni mwandishi wa habari na amewahi kutumikia vyombo mbalimbali vikiwamo magazeti ya Jambo Leo na Mwananchi.

Moja ya changamoto ambazo anaziona katika uandishi wa habari anasema ni pamoja na kuingia mtaani kusaka habari kwani mvua, jua vyote ni vyako.

Hata hivyo baadhi ya makosa anayoyaona kwenye uandishi wa habari, anasema ni pamoja na kutoichimba habari kwa undani na wengine wanaifanya si kwamba wanaipenda kutoka moyoni, bali ni kwa kuwa wamekosa kazi za kufanya.

Mmoja wa wanahabari ambao wamekuwa wakimvutia na kuingia katika fani hiyo anasema ni marehemu Rehema Mwakangale.



Chanzo: mwananchi.co.tz