Rapa T.I. amefunguka kuhusu mwenendo wa mwanaye King Harris ambaye kipindi cha hivi karibuni amekuwa akikosolewa kwa kuwa na tabia mbaya mbele ya Jamii.
Kama utakumbuka September mwaka 2022, King Harris alikamatwa kwa kuvunja sheria za Usalama barabarani ambapo alikutwa na kosa la kutovaa mkanda wakati akiendesha gari, ukiacha makosa mengine kama la kuwahi kumpiga muhudumu wa mgahawa mmoja Jijini Atlanta.
Mikasa hiyo ya King Harris ilimfanya T.I. atoke hadharani na kusema kwamba, mwanaye huyo ataishia gerezani kama hataamua kubadili tabia yake.
Sasa kwenye mahojiano mapya na Shannon Sharpe wiki hii, T.I. amemzungumzia King Harris na kumtetea kwa kusema “Sisi kama wazazi, kati ya watoto wetu wote, tunao watoto waovu na wasiosikia. Nampenda licha ya yote ambayo anapitia, ni Kijana mzuri lakini vyombo vya habari haviongelei mambo mazuri, siku zote wanaanika maovu tu.”