Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

T.I: Young Thug atashinda kesi yake

Ti Salutes Young Thug For Showing Him Gratitude 1191x675.png T.I: Young Thug atashinda kesi yake

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa T.I anaamini Rapa Young Thug atashinda kesi inayomkabili na atarudi nyumbani kama kawaida, mkali T.I amefunguka kupitia mahojiano na kipindi cha radio cha “The Breakfast Club” siku ya Jumanne Mei 28, 2024.

T.I amesema ya kuwa, Rapa Young Thug atarudi nyumbani na kuendelea na maisha yake kwa sababu mpaka sasa waendesha mashtaka hawajapata ushahidi juu ya kesi inayomkabili “Sidhani kama mashahidi ambao wamewaita hadi sasa wamethibitisha kile walichosema” Alisema Rapa T.I

Imetimia miaka miwili sasa tangu Rapa Young Thug awe chini ya ulinzi na kufunguliwa kesi dhidi ya umiliki makundi yanayojihusisha na shughuli za uhalifu, Thug na wenzake walikamatwa na polisi Mei 2022, mpaka sasa kesi inayomkabili inaendelea kusikilizwa mahakamani.

Young Thug ni mwanzilishi na mmiliki wa lebo ya muziki inayojulikana kama “YOUNG STONER LIFE RECORDS” YSL inayomiliki wasanii kama Gunna, NBA Young Boy, Lil Duke Na Wengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live