Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

T.I, Rotimi vita nzito, Wamarekani waingilia kati

Rotimi Ti T.I, Rotimi vita nzito, Wamarekani waingilia kati

Tue, 13 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa ni siku chache baada ya timu ya kandanda nchini Marekani, Atlanta Falcons kumpa kandarasi fupi msanii maarufu wa muziki nchini humo ili Rotimi kuwatungia wimbo kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa kandanda nchini humo.

Rotimi ambaye ni mpenzi na mzazi mwenzake na Vanessa Mdee hakulaza damu, alifanya kweli na kuingia kwenye studio na kurekodi dude moja kwa jina Rise Up kuwasifia wachezaji na timu nzima ya Atlanta Falcons.

Ila hakujua kwamba hatua ya kufanay wimbo kwa ajili ya timu ya Atlanta ndio ungekuwa mwisho wake yeye kutukanwa vibaya na wasanii wengine.

Itakumbukwa msanii huyo ambaye ana asili ya Kiafrika, wazazi wake wote wanatokea Nigeria na huko Marekani wanaishi katika mitaa ya New Jersey.

Sasa wakaazi wa eneo la Atlanta wamefunguka kwenye mitandao ya kijamii wakisema kwamba hatua hiyo haikufaa kwani timu hiyo ingewatumia wasanii kadhaa waliopo Atlanta na si kumleta mtu kutoka jimbo tofauti.

Rapa T.I amekuwa ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao wamejipata katika zogo hilo baada ya kuenda ‘live’ kwenye mitandao yake ya kijamii na kutamka maneno mabaya ya kudhalilisha dhidi ya Rotimi.

T.I katika kipande cha video ambacho kimesambazwa mitandaoni anaonekana akimbagua Rotimi wazi wazi kwa kusema kwamba kando na kuwa si mzaliwa na mkaazi wa Atlanta, lakini pia bado haitoshi yeye ni mtu kutoka nje kabisa ya Marekani.

Matamshi ya T.I yamezua ghadhabu miongoni mwa Wamarekani Weusi ambao wamemjia juu kwani licha ya yeye kuwa Mmarekani mweusi ambaye anafaa kuungana na Wamarekani Weusi wenzake kupigana vita dhidi ya ubaguzi wa rangi ya Ngozi, lakini bado ndiye anakaa mstari wa mbele kumbagua mtu mweusi kama yeye kisa kunyimwa kandarasi ya kufanya kazi na badala yake kukabidhiwa mwanamuziki huyo.

“Mbona mnampa mchongo mtu ambaye si kutoka jiji hili, si tu kutoka kwa jiji hili ila pia kabisa kutoka nje ya nchi,” T.I alionekana akitapika utumbo huo.

Wamarekani wengine walisema wamemsamehe T.I kwa kuelewa kwamba pengine alizungumza hivyo kutokana na hasira za kunyimwa mchongo huo ila pia wengine wakasema kwamba vita dhidi ya ubaguzi wa rangi ya ngozi haswa katika majimbo ya Marekani itakuchukua muda mrefu sana kumalizika kwani watu Weusi wenyewe wanachukiana wenyewe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live