Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sura ya chombo kipya cha Jux bado ni kitendawili

Jux Na Baby.png Jux na mpenzi wake

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Juma Jux, bado amezidi kuifanya kitendawili sura ya mpenzi wake mpya ambaye amekuwa akiposti picha mbalimbali akiwq naye huku mwanamke huyo akiwa aonekani sura yake.

Licha ya Jux na mrembo huyo, kuposti picha zao kwenye akaunti ya instagram ya Jux lakini sura yake haijawahi kuonekana. Mashabiki na wadau mbalimbali wa wapenzi hao wamebaki wakijiuliza. Mwanamke huyo ni nani na kwa nini sura yake haionekani.

Haijulikani ni kwa nini anamficha  sura yake licha ya matamanio yaq wengi kutaka kujua ni mwanamke gani huyo ambaye kwa sasa ameuteka moyo wa Jux baada ya kumwagana na Msanii Mwenzake Vanessa Mdee.

Kupitia Instagrama yake Jux, ameonyesha kutekwa sana na mpenzi wake huyo ambapo mara kadhaa ameonekana kumpost na kuandika maneno ambayo yanaashiria kuwa wawili hao wapo kwenye mahaba mazito.

 "I love you" pia akiwauliza kuwa "Ni mara ngapi kwa siku Huwa unamwambia mpenzi wako I love you" huku akiambatanisha na picha vile vile video akiwa na mpenzi wake.

"So Jana (yaani February 14) ilikua valentine's day na nikamuahidi mpenzi wangu kuwa tutasafiri.Nikamuambia kuwa akajiandae nitampitia kwake. "Alivyomaliza kujiandaa nikampitia, tupo njiani nikamuambia kuwa Kuna kitu nimesahau tunatakiwa kurudi nyumbani.

"Alichokua hafahamu ni kuwa, Kuna surprise Nimemuandalia.????alivyofika nyumbani na kukuta surprise kidogo azimie???? Happy valentines baby, pole kwa Mshtuko ulioupata.

"Nimetumia siku ya valentine Jana kukuonesha ni namna Gani nathamini uwepo na upendo wako Kwangu. Wewe ni mwanamke mrembo sana, Smart, muelewa na najivunia Kuwa na wewe kwenye safari hii ya mapenzi. "Thinking about you Makes it easy for me to write 1000 love song❤️ I love you mi cielito❤️. Aliandika Jux.

Unaweza kutuambia unahisi mpenzi mpya wa Jux ni nani? Usikose kufuatilia Dondoo za Mimi Na Uhusiano kila Jumapili kupitia Kipindi cha Barizi On Sunday, TBC FM 90.0 kuanzia saa 3 hadi saa 6 mchana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live