Menu ›
Burudani
Mon, 22 Jan 2018
Chanzo: bongo5.com
Ni jumapili nyingine nakuletea nukuu kutoka kwa watu ambao wamefanya mambo makubwa au ya kipekee katika ulimwengu huu, Nukuu za leo zimelenga kukujengea imani (belief) kuelekea mafanikio yako.
- Ili kufanikiwa ni lazima kuamini kwanza katika yale tunayoyaweza – Michael Korda.
- Kile ambacho akili ya mtu inaweza kukipokea na kikiamini, akili (yeye) yake inaweza kukifanikisha – Napoleon Hill.
- Ishi katika imani yako na unaweza kuubadili ulimwengu unaokuzunguka –Haenry David Thoreau.
- Amini katika kile unachokifanya na sio kile watu wengine wanachosema –Jacob Geit Dekker.
- Imani yako itaonyesha matendo yako, na matendo yako yataonyesha matokeo. Lakini cha kwanza ulichokuwa nacho ni imani – Mark Victor Hansen.
- Hatu ya kwanza na muhimu kuelekea mafanikio, ni kuhisi au kuamini kuwa tunaweza kufanikiwa – Nelson Boswell.
Chanzo: bongo5.com