Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sukari ya Zuchu labda kwenye kahawa ila sio chai

Zuchu Pic Data Sukari ya Zuchu labda kwenye kahawa ila sio chai

Wed, 3 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

KWA kawaida chai hunyweka na mtu yeyote bila kujali ni mkubwa au mtoto ila kahawa mara nyingi hunywewa na watu wazima hasa nyakati za jioni ili kuwaondolea uchovu baada shughuli za kutwa nzima.

Sukari inatumika zaidi kwenye chai na watoto hupenda kutia nyingi katika kikombe kama hakutakuwepo na uangalizi wa mzazi au mlezi. Ila kwenye kahawa ni watu wazima wachache hupendelea. Hii ni kinyume kabisa na Sukari ya Zuchu ambayo inaonekana inahitajika zaidi kwenye kahawa kuliko chai.

Mwimbaji huyo wa mwisho kusainiwa na lebo ya WCB Wasafi ameufungua mwaka kwa kuachia wimbo uitwao Sukari ambao umepata mapokezi makubwa zaidi.

Ndani siku mbili umeweza kusikilizwa zaidi ya mara milioni mbili kwenye mtandao wa YouTube na kushika nafasi ya kwanza.

Hata hivyo, Zuchu mwenyewe anatoa tahadhari kwa wakubwa wenzie kuhusu Sukari hiyo kwa sababu wakiizidisha hata kijiko kimoja itawapoteza kabisa na hata yeye anaiogopa.

“Nikitaka kusitisha ananiambia ongeza, japo imethibitishwa ila itampoteza,” anasema Zuchu mwanzoni kabisa mwa wimbo huu uliotayarishwa na Prodyuza Laizer.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz