Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Sukari Guru inakaza uke, mwanamke usitumie kidole - Kungwi

Kungiw Mama Mama Love Kungwi

Thu, 17 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkufunzi maarufu wa masuala ya ndoa Mama Love Kungwi ameeleza kuwa, wanawake wanaotumia dawa zenye kemikali ili kutunza maumbile yao wanajitafutia matatizo ya afya kwani kuna njia nyingi za asili ambazo hazina madhara kwa afya zao.

Mama Love Kungwi amesema hayo wakati akihojiwa na Diva The Bawse katika kipindi cha Lavidavi kupitria Wasafi FM.

"Wanawake wasitumie kemikali, watumie vitu vya asili, Sukari Guru ni nzuri ukiitumia inasaidia kukaza kuta za uke. Mwanamke usafi muhimu sana, maji ya baridi ni mazuri sana kwa Mwanamke kusafisha maumbile yake.

"Mwanamke usitumie kidole chako kuingiza ukeni wakati unajisafisha. Hii inakuwa sababu za kuingiza vijidudu vya magonjwa. Kama utatumia iwe mara chache sana na kwasababu maalum.

"Mwanamke unapofanya mazoezi unapata faida ya kuwa mwepesi kwenye tendo ... Mpenzi wako hatakuona mzigo kitandani.

"Watu wengi hawana utaratibu wa kuoga kabla ya tendo. Hakikisha unaoga kabla na baada ya kufanya tendo hii inasaidia kutunza maumbile yako," amesema Mama Love Kungwi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live