Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sugu: Ugomvi Wangu na Ruge Ulikuwa ni wa Kibiashara

Sugu88 Sugu: Ugomvi Wangu na Ruge Ulikuwa ni wa Kibiashara

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MMOJA wa waasisi wa game ya Hip Hop Bongo kwenye mfumo wa kuwa kibiashara, Joseph Mbilinyi 'Sugu' ambaye kwa sasa amerudi kwenye game na goma lake la TAITA aliyomshirikisha Billnass ameweka wazi kuwa hajawahi kumiss jengo la bunge bali anacho-kimiss ni kusimama kule ndani na kuwaongelea watu wake wa Mbeya.

Sugu ambaye amewahi kuwa mbunge wa Mbeya Mjini kwa miaka 10 amedai kuwa hapendi kuongelea ugomvi wake na aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, marehemu Ruge Mutahaba kwani tayari alishatangulia mbele ya haki, hivyo ataonekana mnafiki.

Sugu amesema kwa kifupi ni kuwa ugomvi wao ulikuwa wa kibiashara zaidi na sio mambo binafsi na ndio maana Ruge alipokuwa akifika Mbeya hufikia kwenye hoteli yake (Sugu) na wakaongea mambo mbali mbali ya kimaendeleo.

Akizungumza kwenye mahojiano yake na XXL ya Clouds Fm, jana Februari 17, Sugu alisema; "Kilicho tokea ni kuwa nilijaliwa kujua mengi zaidi, hata lilipokuwa linakuja suala la kupanga vitu hususani vya kwenye game.

"Nikiwa anauliza au kutoa hoja zinazokinzana na maoni ya mabosi basi nilionekana kama najua sana hivyo wakawa wanniweka pembeni wanaondoka na wale wa ndio ndio, kwa hiyo yalikuwa ni mambo ya biashara zaidi," alisema Sugu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live