Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sugu: Sijasoma sana ila nimetoboa

Suguuu Mr II Sugu.

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii mkongwe Tanzania Mr II Sugu amesema hata yeye hajasoma sana elimu ya darasani lakini ametoboa kiaina kwenye maisha.

Sugu amefunguka hilo baada ya kupost picha ya msosi wa samaki, ndizi na salad kisha kuandika "Mlipokuwa mnaambiwa msome Elimu ni ufunguo wa maisha mkaleta ubishi sasa mnabaki mnatamani tu".

Mashabiki wengi wamemjia juu suala hilo la msosi na elimu wakimuhoji kwamba vinaingiliana vipi katika maisha ambapo amewajibu hata yeye hajasoma elimu ya darasani lakini ametoboa.

"Haya isiwe tabu bandugu, Mie mwenyewe sijasoma Elimu ya darasani kiivyo na nimetoboa kiaina" ameandika Sugu kwenye post yake mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live