Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Str8up yatoa kauli Kizz Daniel kuingia mitini shoo ya Dar

Kizz Daniel Str8up yatoa kauli Kizz Daniel kuingia mitini shoo ya Dar

Mon, 8 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Str8up Vibes ambao ndiyo Waandaaji wa Tamasha la Summer Amplified wametoa tamko kufuatia Msanii wa Nigeria Kizz Daniel kushindwa kutotokea kabisa ukumbini kutumbuiza usiku wa kuamkia leo kama ilivyotakiwa na kupelekea Mashabiki kukasirika.

Taarifa ya Str8up Vibes leo imesema; "Sisi katika Str8up Vibes tunasikitika sana kwa kilichotokea kwenye Tamasha la SUMMER AMPLIFIED Aug 07 2022 ambapo Kizz Daniel hakutumbuiza kama ilivyotarajiwa.

"Tunakubali kwamba hii imesababisha kuvunjika moyo kwa Wateja wetu waaminifu na Wadau muhimu wa muda mrefu waliohusika, tunachukua hatua zinazofaa katika kushughulikia suala hili kwa ukali na kuuhakikishia Umma na mashabiki waliolipa na kuhudhuria kwamba tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha tunaweka hali vizuri, tunaomba subira yao tunaposhughulikia hili"

"Str8up Vibes ni kampuni inayoheshimika na iliyojijengea sifa thabiti, kuridhisha Wateja wetu siku zote imekuwa jukumu letu kwa miaka mingi ambayo tumekuwa katika biashara hii, tutawasiliana kwa hatua zaidi zinazofuata, Ahsante kwa kuelewa" - Damian Mapala, Mkuu wa mawasiliano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live