Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stevie Wonder achukua Uraia wa Ghana

Lumii 20240513 175450874 Edited Stevie Wonder achukua Uraia wa Ghana

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki kutoka Marekani Stevie Wonder sasa anatambulika kama raia wa Ghana, hii ni baada ya kula kiapo cha Utii na kupokea cheti cha Uraia kutoka kwa Rais wa nchi hiyo Nana Akufo-Addo siku ya jana Mei 13, 2024.

Mkali huyo wa R&B ambaye amezaliwa katika jimbo la Saginaw, Michigan, Marekani, alikula kiapo hicho katika siku yake ya kuzaliwa, jana Mei 13 akiwa anatimiza miaka 74 katika Ikulu ya Jubilee jijini Accra nchini Ghana.

Stevie Wonder siyo msanii pekee ambaye amekuwa akiutaka uraia wa Ghana kwani mwanamuziki Meek Mill naye ni mmoja wa wasanii ambao wanaitaji uraia wa nchi hiyo na kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali vinaweka wazi kuwa huenda ‘rapa’ huyo naye akakubaliwa kuwa raia wa #Ghana siku chache zijazo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live