Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Steve RnB: Akina Kizz Daniel wameshiba kiburi

Steve Na Kizz Steve RnB: Akina Kizz Daniel wameshiba kiburi

Tue, 9 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii maarufu wa Bongo, Steve RnB ameibuka na kuzungumzia sakata la supastaa kutoka nchini Nigeria, Oluwatobiloba Daniel Anidugbe maarufu kama Kizz Daniel kukacha shoo ya Summer Amplified aliyotakiwa kufanya usiku wa kuamkia jana Agosti 8, 2022 jijini Dar.

Inaelezwa kuwa, Kizz aligoma kufanya shoo hiyo kwa sababu ya kutokuwepo nguo zake ambazo kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali ni kuwa alisahau nguo hizo nchini Kenya.

"Jamani tuamkenii wadau wa muziki mtu analipwa pesa nyingi anakuja kuvimba tu hotelini Bongo, kisa sababu eti nguo hazihafika. Wakati wasanii wa kali tunaachwa nyuma kwa kuwakimbilia hawa wageni duh! Halafu eti wamempa millions of dollars.

“Tukomaeni na vipaji vyetu vya hapa nchini hawa jamaa hawajali chochote, wameshiba kiburi, muziki wetu ukipewa kipao mbele ni mkali kuliko hata hao watu wanaokimbilia now days!" amesema Steve.

Kizz Daniel ambaye ni hit-maker wa wimbo wa Buga kutua kwenye ardhi ya Tanzania staa huyo hakufanikiwa kufanya shoo hiyo jambo lililosababisha kukamatwa na kupelekwa katika kituo cha Polisi Oysterbay ambapo alishikiliwa kwa saa kadhaa kabla ya Harmonize kumwekea dhamana na kumtoa lupango.

Licha ya Kizz kutotokea jukwaani mastaa wengine kutokea nchini Tanzania kama Marioo, Saraphina, Mabantu na Young Lunya walifanikiwa kutoa burudani kwenye shoo hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa #WareHouse zamani Nextdoor.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live