Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Steve Nyerere atoa neno kipigo cha Amber Lulu

Nyerere Na Amber Steve Nyerere atoa neno kipigo cha Amber Lulu

Tue, 17 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kusambaa kwa taarifa ya kushushiwa kipigo kwa msanii Amber Lulu na video yake kusambaa mitandaoni, muigizaji Steven Mengere 'Steve Nyerere' naye ameshusha waraka wake mtandaoni juu ya ishu hiyo.

"Kwanza kabisa nakupa pole sana wewe ni binti unayeangaika kweli kwa ajiri ya family yako, Naimani hata hicho kipato unachopata ni kidogo sana kulingana na family iliyo kuzunguka.

Jina lako ni kubwa na unayo pitia ni ngumu kuamini Dada ila Dada siku zote Mapenzi yanamwisho, Mimi sitaki kuamini kama Mwanamke unaweza kumrekebisha Tabia kwa kumpiga Apana.

Najiuliza mwanaume ambaye umezalisha halafu husimamii majukumu kama baba kuhakikisha aliyeingia Leba na kuriski maisha yake ni kweli leo zawadi yake ni makofi au kipigo.

Unapata wapi nguvu ya kumpiga mzazi mwenzako tena yawezekana anatafuta chakula cha mtoto pamoja na wewe huyo huyo.

Kama Kweli unampenda ungeleta ugali ungeona kama angekuwa anatoka... Dada zetu wengi walimiliki upendo na kufanya maamuzi Magumu ya kuzaa na watu wa hovyo sana.

Mchukulie hatua kali sana, nenda karipoti Police ???? Ipo siku Atakupiga utajikuta unakufa kwa kipigo ukiacha mwanao anateseka kwa upumbavu tu. Sifa ya mwanaume yoyote yule Duniani ni kutunza kile unacho miliki.

Mwanaume anayekaa na mwanamke au kuzaa naye atasifiwa kwa kumtunza mkewe hakikisha mahitaji ya mkeo yapo, anapendeza, na lazima ujue majukumu yako kwa mwanamke wako.

Ni ushamba sana kwa Duniani ya leo kupiga mwanamke. Vikishindikana ni bora mbaki na ile kauli mzazi mwenzangu yule basi inatosha. Kipigo kwa mwanamke hakikubaliki kabisa.

Tusilifumbie macho hili kuona dada zetu wanateseka kwa kutafuta riziki na wakirudi nyumbani wanakutana na unyama wa kipigo..

Mwanaume anasifiwa kutunza mkewe, mchumba, sio kumfanya punch ???? bag ???? ???? ????, Dada nitasimama na wewe, pole sana nimejisikia vibaya sana, najua unavyopambana kupitia kipaji chako na bado unabaniwa halafu unarudi home unakutana na fala ananyanyua mkono kukupiga wakati yeye mwenyewe hasimami kama baba..

Huuu ukatili sana haukubaliki kabisa. Dada ulipo nipo pole sana. Ila ni funzo kwa dada zetu wengine muangaliage na watu wa kuzaa nao kaaaaa. Nenda dawati semaaaa. Nenda.

Tusije siku tukatoa maiti siku. Mwanamke hapigwi. Anaelewashwa. Tutafute hela jamani wanaitaji matunzo bahati mbaya Marioooo wamekuwa wengi sana sasa wanafanyia umarioo mpaka maskini wenzao."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live