Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Steve Nyerere atoa gari la kusafirishia mwili wa Erick Kisauti

Steve Nyerere Erick Steve Nyerere atoa gari la kusafirishia mwili wa Erick Kisauti

Fri, 19 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwili wa Mchekeshaji Erick Kisauti umeagwa jana Kibaha, Pwani na Wasanii na Wadau mbalimbali kabla na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Mwanza kwa ajili ya maziko.

Hapo awali kulikua na changamoto ya fedha iliyopelekea kuitisha michango ili mwili huo usafirishwe ambapo hata hivyo Mwigizaji Steve Nyerere @stevenyerere2 aliingilia kati na kujitolea gari la kuusafirisha mwili wa Mwigizaji huyo huku Wadau mbalimbali wakitoa michango mingine mbalimbali.

Mchekeshaji Sobogani Zablon maarufu Erick Kisauti alifariki alfajiri ya August 17 akiwa nyumbani kwa Ndugu zake Kibaha, Pwani na anatarajiwa kuzikwa Mwanza August 19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live