Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Steve Nyerere aomba umoja kwa wasanii

C02e0f2b44bbacefbd18dc1fe4d20d33.jpeg Steve Nyerere aomba umoja kwa wasanii

Sat, 20 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MWIGIZAJI mkongwe Steven ‘Nyerere’ Mengele amesema ni jukumu lao kama wasanii kusimama na kuonesha umoja wao na uzalendo kwa taifa kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya Rais wa awamu ya tano John Magufuli.

Magufuli alifariki dunia Jumatano ya wiki hii Dar es Salaam kutokana na maradhi ya moyo.

Katika ujumbe alioandika Steve kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, alisema anaamini wasanii wenzake wanaelewa nini maana ya msiba hivyo hatarajii kuona wanatumia vibaya.

“Ninaimani hakuna asiye jua tunapita kwenye kipindi gani basi ni jukumu letu kusimama na kuonesha umoja wetu na uzalendo wetu kwa Taifa letu, sitarajii kuona au tukaona kiki au mambo ya ajabu kwenye mitandao yetu,”alisema.

Alisema Magufuli alikuwa kiongozi shupavu kwa Taifa hivyo ni muda wa kuungana na watanzania wengine kwenye kipindi hiki cha majonzi.

“Wenye kutunga nyimbo, mashairi, wachoraji, wacheza sinema, mziki wa dansi wote kwa pamoja tushirikiane kwenye hili, ni ngumu kuamini lakini kwa Mungu kila jambo linawezekana,Tushirikiane kwa maombi na sala,”alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz