Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Steve Nyerere amwangushia tusi zito Manara

Manara Steve Steve Nyerere na Manara

Mon, 25 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Steve Nyerere au Tivu Ake; ni komediani wa Bongo Movies ambaye ameshindwa kuvumilia masiahara ya Semaji la Yanga, Haji Manara na kujikuta akimpa tusi.

Steve ameposti picha ya binti yake mkubwa kisha akaandika; “Tafuta muda wa kukaa na familia, kujifanya upo bize hakusaidii kama familia haikuoni. Rafiki wa kwanza kwenye maisha yako ni familia yako…”

Baada ya hapo, mashabiki wake walianza kutoa maoni mbalimbali huku Manara akiandika; “Chuma changu cha tatu mashallah…”

Kitendo kinaonekana kumkera Steve ambaye amejikuta akimjibu Manara kwa tusi kwa kumuambia; “Achaga ….(tusi) basi kaaaaaa…”

Wachangiaji wengine walidai kuwa Steve atakuwa amemaindi baada ya Manara kumtania kuwa atamuoa mwanaye mke wa tatu baada ya hivi karibuni kuoa mke wa pili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live