Steven Mengere 'Steve Nyerere' amekataa uchungaji kisa Zumaridi kwa kusema anatamani Uislamu kutokana na jinsi watu wanavyoichukulia poa dini ya Kikristo.
Msanii huyo wa filamu na Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza amedai ataendeleza kampeni yake ya kupinga wachungaji aliowaita ‘wa mchongo’ kutokana na sakata la Mchungaji Zumazidi ambaye amekuwa gumzo kutokana na kauli zake za kuwa amekwenda mbinguni na kukutana na Mungu.
Steve amedi anaheshimu sana Uislamu kwa kuwa hauchezewi tofauti na dini zingine ambapo ametamani hata kubadili dini.
“Nitaitwa Salim, mimi sitafuti kiki, baa zimegeuzwa makanisa. Sisi tulikuwa tunaishi kwenye imani ya Kikatoliki, tunafundisha watoto utii wa imani lakini leo hii mtu anaibuka tu na kusema lolote kuchezea dini,” alisema Steve Nyerere.