Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Steve Nyerere: Nitaamuunga mkono MwanaFA mpaka peponi

NYERERE SIPINGI Steve Nyerere: Nitaamuunga mkono MwanaFA mpaka peponi

Thu, 2 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchekeshaji Steven Mengere 'Steve Nyerere' amesema atahakikisha anamuunga mkono Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma 'MwanaFA'.

Nyerere ametoa kauli hiyo Marchi Mosi, 2023 alipokuwa akifanya mahojiano na Clouds FM Radio ambapo alieleza mambo mbalimbali ikiwemo kutofautaiana na MwanaFA ambaye aliteuliwa kushika wadhifa huo na Rais Samia Suluhu Hassan, Jumapili iliyopopita.

“MwanaFA ni mteule wa Rais, Rais ndio kamuona anafaa kuwa pale na kumfanya kuwa kiongozi wetu mimi ni nani nipinge uteuzi wa Rais! Mimi ni nani nigombane na mteule wa Rais!? Embu vaeni viatu vyangu muwe nyinyi! Natakiwa kumuunga mkono mwanafa mpaka anaenda peponi,” alisema Steve Nyerere.

Nyerere aliwahi kugombana na MwanaFA kufuatia kuteuliwa kuwa Msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania ambapo, MwanaFA alipiga Nyerere kushika nafasi hiyo na alifanikiwa kwani mchekeshaji huyo alijiuzulu siku chache baada ya kuteuliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live