Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Steve Nyerere: Niliwekewa sumu kwenye kitimoto

Steve Nyerere: Niliwekewa Sumu Kwenye Kitimoto Steve Nyerere: Niliwekewa sumu kwenye kitimoto

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji Steven Mengere 'Steve Nyerere' amesimulia mambo mbalimbali yaliyowahi kumtokea pindi aliojihusisha kwenye masuala ya siasa 2020 ikiwemo ishu ya kuwekewa sumu kwenye chakula.

"Niliwekewa sumu kwenye kitimoto (nguruwe). Aliyeniwekea sumu nilimtambua. Nilimjua na nimemsamehe! Hicho chakula tulikula Mimi na JB.

"(JB mroho!) Yeye alipokiona kile chakula alikivamia. Tulipomaliza kampeni za uchaguzi Mkuu wa 2020. Baada ya mwezi mmoja nilimwita sehemu Moja hivi. (Sehemu waliyokula chakula)

Yeye mwenzangu kwa kuwa ana mwili mnene hadi ile sumu isambae mwilini ilichukua muda mrefu. Baada ya siku Nne. Nililazwa hospitali ya Kairuki kwa muda wa Miezi Miwili," alisimulia Steve Nyerere.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live