Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Steve Nyerere: Nandy na Billnass sio harusi, nawaonya wazamiaji

Nyerere Steve Uteuzi Steve Nyerere, Nandy na Billnass

Sat, 2 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa ni siku mojaa baada ya kuchaguliwa kwa msanii maarufu nchini, Steve Nyerere ibu ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Harusi ya wasanii wenzake, Billnass na Nandy, hatimaye Steve asiyeishiwa vituko amekuja na jipya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Steve amewashukuru Billnass na Nandy kwa kumpa heshima hiyo ya uenyekiti huku akiahidi kusimamia harusi hiyo na kuwa ya viwango vya juu.

"Billnass na Nandy nichukue nafasi hii kusema asanteni sana, nimekaa nimelitafakari ombi lenu nimelichambua kwa kina nikasema ya nini nikatae, ndoa ni jambo kubwa na baraka pia.

“Niseme tu hiii sio harusi, ni wedding watu wengi wanafanya harusi, sisi tunaenda kufanya wedding. Ni wedding ambayo toka uhuru wa taifa hili haijawahi kutokea.

“Nyie hamuendi kufanya harusi mnafanya wedding chini ya usimamizi wangu, asanteni sana. Niwape onyo wazamiaji, wedding day hatukagui kadi tunakaribisha watu na Watanzania,'' amesema Steve.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live