Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Steve Nyerere: Lulu kaleta heshima kwa wasanii

45c30a03862846e6b68cde97b7278752 Steve Nyerere: Lulu kaleta heshima kwa wasanii

Thu, 18 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MWIGIZAJI mkongwe wa filamu na sanaa ya vichekesho, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ amesema kitendo cha Elizabeth Michael ‘Lulu’ kufunga ndoa kimeleta heshima kwenye sanaa hiyo.

Lulu alifunga ndoa juzi na mchumba wake wa muda mrefu, Francis Cizza ‘Majizzo’ ambaye ni mmiliki wa kituo cha redio cha Efm na televisheni TVE katika Kanisa Katoliki la Mt Gasper Mbezi Beach, Dar es Salaam.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Steve Nyerere aliweka picha za ndoa na msanii huyo na kuandika ujumbe huu:

“Uhuru unakuja kesho haya Elizabeth Michael kamaliza kila kitu kaleta heshima kwenye kiwanda cha filamu, hongera sana, uvumilivu ni mtaji mkubwa, sijajua anayefuatia? Mwenzenu ndio huyo kuanzia leo ni Mama Majizzo.”

Ujumbe huo aliusambaza kwa wasanii wengine kama Wema Sepetu, Blandina Chagula, Maya Mrisho, Jackline Wolper, Irene Uwoya na Lulu Diva na kuwauliza je, wao lini?

Baadhi yao walijibu ujumbe huo, ambapo Wolper alisema wao tayari bado nguo nyeupe kwani aliogopa vipingamizi.

Uwoya yeye alisema yeye alishamaliza muda sana na kwamba ni mjane kwa sasa, huku Johari akisema ya kwake itafanyika muda sio mrefu na Maya akisema ya kwake alishamaliza.

Chanzo: habarileo.co.tz