Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Steve Nyerere, Irene Uwoya waitikia wito wa Basata

67162 Pic+nyerere

Wed, 17 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wasanii wa Bongo movie nchini Tanzania, Irene Uwoya na mwenzake, Steve Nyerere leo Jumatano Julai 17, 2019 wamefika katika ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kuitikia wito wa baraza hilo.

Wasanii hao wameitwa Basata jana Jumanne Julai 16, 2019 baada ya Uwoya kutumia mkutano wa wasanii  na waandishi wa habari kurusha fedha kwa waandishi jambo lililozua mjadala ikiwamo kuonyesha dharau kwa wana taaluma hao.

Leo, Irene na Steve walitinga katika viwanja hivyo vya Basata saa 4:30 na gari aina ya Toyota Prado nyeusi.

Kabla ya kushuka walikaa zaidi ya robo saa ndani ya gari huku waandishi waliofika hapo wakiwa wametegesha kamera zao kusubiri kuwachukua picha.

Ilipofika saa 4:45 asubuhi wasanii hao walishuka kwenye gari hilo na kuelekea ndani ya ofisi ya Katibu Mtendaji wa Basata.

Chanzo: mwananchi.co.tz