Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stara atoa sababu ndoa za wasanii kuvunjika

Starah Stara atoa sababu ndoa za wasanii kuvunjika

Mon, 22 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKONGWE wa muziki nchini, Stara Thomas, amesema ndoa nyingi za wasanii zinavunjika kutokana na kutokuaminiana wenyewe.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Stara alisema, wasanii wengi wanakurupuka kuingia kwenye ndoa wakiwa bado hawajajipanga ndio maana wanashindwana.

“Ndoa nyingi huwa zinavunjika kwasababu ya kukosekana kwa uaminifu na si pesa wala mali kama wengi wanavyoamini.

“Kila mmoja anakuwa hana imani na mwezake, kitu hicho hakiwezi kujenga uhusiano mzuri wala familia bora, lazima mwisho wa siku itavunjia, watu wajifunze kuwa waaminifu itawasaidia kwenye maisha yao,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live