Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stara Thomas afunguka “Nipo kimya ila ninaishi”

Stara Thomas Stara Thomas

Thu, 5 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

“Wengi nimewaona ila moyo… Watakapo tuuu kutulia… Kwa dhati ninanena Ukweli ninasema…aahh kutoka moyoni… Nipo kwa ajili yako wewee… Hata kama uende mbali ohhh…

Sito linadi pendo lako…

Hivyo ndivyo nilivyo bwana weehh…

Hata kama waseme sana…

Nipo kwa ajili yako weehh…

Hata kama wanune sana…

Nipo kwa ajili yako weehh…

Hata kama wasuse sana…

Nipo kwa ajili yako weehh…

Nipo kwa ajili yako weehh…

Fahari ninapata uwapo karibu yangu ohh…

Kila wakati oohh…

Siku hadi siku wazidi kutulia aahh…

Moyoni mwangu…

Shaka sikutilii weweee…

Kwani jibu nimeshapata yoohh…

Nafsi imekubali nayooo…

Kipingamizi hakuna tena yoohh…

Hata kama waseme sana…

Nipo kwa ajili yako weehh…”

Haya ni mashairi ya Ngoma ya Nipo Kwa Ajili Yako. Ni moja kati ya ngoma kali kutoka kwa mwanamama mkongwe muziki nchini Tanzania, mama wa makolabo, Stara Thomas.

Ni mama wa makolabo kutokana na baadhi ya ngoma zake kushirikiana na wasanii wengi na nakufanya vizuri kama Riziki ya K Basil na Bizman, Kigugumizi ya Mr Paul, Ungeniambia ya MwanaFA, Mchakamchaka ya Mr 2 a.k.a Sugu, Nipigie ya AT na nyinginezo.

Stara anasema anafurahia kufanya ngoma na msanii mwingine kuliko kufanya mwenyewe ndiyo sababu nyimbo zake zote alizoshirikishwa au kumshirikisha msanii yeyote, watu wanazifurahia na yeye mwenyewe anazipenda.

Stara anayasema hayo kutokana kurudi tena rasmi kwenye muziki Bongo Fleva baada ya kufanya muziki wa Injili na kufanikiwa kutoa album moja ya Nani Mshamba.

Anasema hivi sasa anafanya kazi zaidi kwa kushirikiana na wasanii wengine kwa sababu anapenda umoja.

Anasema mikakati yake aliyonayo hivi sasa ni kuachia nyimbo zake back to back ili kuweza kurudisha mashabiki wake kama zamani ingawa anaamini kwamba hawajapotea kutokana na ngoma zake zinavyoishi.

Kuhusu album anasema kuwa alishauriwa kufanya hivyo, lakini halifikirii hilo kwa sasa kwani hakuna mabadiliko yoyote sokoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live