Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stamina afunguka kuhusu kumuomba msamaha mkewe

91624 Pic+stamina Stamina afunguka kuhusu kumuomba msamaha mkewe

Tue, 2 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkali wa HipHop Bongo Stamina, amefunguka na kusema suala la kuombana msamaha na aliyekuwa mkewe ni jambo la siri na watu wawili, kwani wakati wanakubaliana kuwa kwenye mahusiano hakuwaambia watu.

Akifunguka hilo kupitia EATV & EA Radio Digital Stamina amesema "Mimi sijaweka mahusiano yangu wala kumuonyesha mke wangu, ule ni mziki tu halafu sijui kwanini Watanzania hawaamini kwamba naweza nikamuimbia mtu mwingine, nimeongelea ndoa sijamuongelea mwanamke wangu".

"Masuala ya kuombana msamaha ni mambo binafsi ya watu wawili, kama yeye ameomba msamaha au mimi nimeomba msamaha ni vitu binafsi na hata ikitokea hivyo lazima ianze kwa watu wawili siwezi kuja kuvisema hadharani kwa watu".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live