Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stamina: Niko tayari kurudiana na mke wangu

Stamina Pic Data Stamina: Niko tayari kurudiana na mke wangu

Fri, 24 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkali wa Hip Hop Bongo, Stamina amesema, yupo tayari kurudina na aliyekuwa mkewe ambaye waliachana miaka kadhaa iliyopita.

Stamina ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na Clouds FM kuhusu masuala mbalimbali ya maisha yake ambapo alisimulia jinsi alivyoachana na mkewe baada ya kushindwana.

"Kama nilivyosema sipendi sana kutabiria yajayo lakini kama ikitokea tumekaa, tukayazungumza hakuna shinda tunaweza kuishi," alisema Stamina.

Kwenye maelezo yake mengine kwenye mahojiano hayo, Stamina alisema, aligundua umuhimu wa ndoa baada ya kutoka kwenye ndoa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live