Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Staa wa Sauti Sol Ajitangaza Kujihusisha na Mapenzi ya Jinsia Moja

Sauti Shoga Chimano

Thu, 9 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwimbaji maarufu wa muziki wa pop nchini Kenya anayeunda Kundi la Sauti Sol, Willis Austin Chimano amejitokeza kama mpenzi wa jinsia moja.

Chimano ametoa tamko hilo hadharani wakati alipokuwa akielezea wazo la wimbo wake mpya wa 'Friday Feeling', ambapo aliwashirikisha wanajamii wa LGBT.

"Hakuna kujificha tena," aliambia vyombo vya habari vya ndani.

Alisema kwa sasa anaishi ukweli wake na atatumia muziki wake kupinga taasubi za kiume zenye sumu, chuki na unafiki.

Chimano hajawahi kujitokeza hadharani kama mpenzi wa jinsia moja ingawa hapo awali aliwahi kuonekana na wapenzi wa kiume.

Tamko hilo la hadharani linaweza kuwa kupiga jeki juhudi za kupigania haki za watu wa jamii ya LGBT nchini Kenya, ambapo mapenzi ya jinsia moja yameharamishwa na yanaweza kuadhibiwa kwa hadi miaka 14 jela.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live