Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Staa wa Filamu Hollywood afariki Dunia

Staa Wa Filamu Mwigizaji wa Hollywood Donald Sutherland

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji wa Hollywood Donald Sutherland, kutoka nchini Canada aliyejizolea umaarufu kupitia filamu ya ‘The Hunger Games’ na MASH, amefariki dunia siku ya jana nyumbani kwake jijini Miami,Florida nchini Marekani akiwa na umri wa miaka 88 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mtoto wa mwigizaji huyo Keifer Donald (Jack Bauer) ambaye pia ni mwigizaji amethibitisha kutokea kwa kifo cha baba yake huku akieleza namna alivyosikitishwa na msiba huo.

Keifer amesema “Kwa moyo mzito, ninatangaza kwamba baba yangu, Donald Sutherland, ameaga dunia. Binafsi nadhani mmoja wa waigizaji muhimu katika historia ya filamu, lipenda alichofanya na kufanya kile alichopenda”

Sutherland aliwavutia mashabiki wengi kupitia filamu za kivita alizoigeza na kuonesha umahiri mkubwa zikiwemo ‘Kelly's Heroes’, na ’‘The Eagle Has Landed’ .

Mwigizaji huyo alikabidhiwa tuzo ya nyota ya heshima ya ‘The Hollywood Walk Of Fame’ mwaka 2011 kutokana na mchango wake wa kukuza tasnia ya uigizaji nchini Marekani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live