Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Staa wa "Fast Furious" matatani kwa unyanyasaji wa Kingono

Vin Diesel Ngono Muigizaji na producer kutoka nchini Marekani Vin Diesel

Sat, 23 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji na producer kutoka nchini Marekani Vin Diesel anakabiliwa na kesi ya udhalilishaji wa kingono kwa aliyekuwa msaidizi wake aitwaye Jonasson.

Mkali huyo wa 'Fast & Furious' naye ameingia katika orodha ya ma-star wanaokabiliwa na kesi za unyanyasaji wa kingono baada ya #Jonasson kudai kuwa #Diesel alimlazimisha kufanya naye mapenzi bila makubaliano.

Kufuatiwa na nyaraka za kisheria zilizowasilishwa mahakamani zimeeleza tukio hilo lilitokea mwaka 2010 wakati wa uandaji wa filamu ya ‘Fast 5’ ambapo #Jonasson aliajiriwa na kampuni ya ‘One Race’ kama msaidizi wa #Diesel huku nyaraka hizo zikieleza kuwa tukio hilo lilitokea katika chumba cha muigizaji huyo kwenye hoteli ya ‘St Regis’ jijini #Atlanta.

Aidha mwanadada huyo amedai kuwa alikaa kimya muda wote kwa kuogopa nguvu na ushawishi mkubwa alionao muigizaji huyo. .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live