Watayarishaji wa filamu ya Black Panther wamemteua Winston Duke kuigiza nafasi ya Black Panther kama ile ya marehemu Chadwick Boseman baada ya mwanadada Letitia Wright kushindwa kufika Marekani kutokana na kukataa chanjo ya Virusi vya Corona.
Kufuatia kifo cha muigizaji Chadwick Boseman wa Black Panther, watayarishaji wa filamu hiyo waliumiza kichwa kumpata mrithi atakayecheza uhusika wa marehemu Chadwick Boseman na hatimae wakampendekeza mwanadada Letitia Wright ambaye aliigiza kama Shuri kwenye sehemu ya kwanza ya filamu hiyo.
Lakini taarifa za ndani zinaeleza kuwa watayarishaji wa filamu hiyo wameamua kuachana na Letitia Wright na kumpendekeza Winston Duke kuchukua nafasi hiyo!
Siku chache zilizopita vyombo vya habari viliandika kuwa , utengenezaji wa filamu ya Black Panther umesimama kutokana na kuumia kwa Letitia wakati wa utengenezaji wa filamu hiyo, huku taarifa zikieleza kuwa filamu hiyo inatayarishwa Atlanta nchini Marekani, ambapo kuna katazo la watu wasiopata chanjo ya Corona kufika nchini humo.
Winston Duke na Letitia Wright nani ataitendea haki nafasi ya Chadwick Boseman?