Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Oxlade amedai alishindwa kumaliza chuo mwaka wa mwisho kwa sababu ya kuzongwa na mambo ya kishirikina.
Mkali huyo aliyetamba na wimbo wa ‘Kulosa’ ambaye alisoma Chuo Kikuu cha Lagos (LASU) anadai kuwa rafiki yake alimfuata na kumwambia wajiunge katika genge la kuabudu mashetani hivyo yeye alikataa kwa kuwa anamuamini Mungu tu na kupelekea aache chuo.
Kufuatia mahojiano yake na Tea with Tay podcast, ‘staa’ huyo ameeleza kuwa wakati yuko chuo siku zote alikuwa kanisani akisoma ‘biblia’ na vitabu vya dini ila aliacha chuo mwaka wa mwisho kwa sababu marafiki zake walikuwa wakimshawishi ajiunge na gele la kuabudu mashetani jambo ambalo yeye hakulitaka kulifanya.