Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spika aibana Serikali kuzuia tamasha la Bobi Wine

32337 Bobipic Bobby Wine

Wed, 19 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kampala, Uganda. Spika wa Bunge la Uganda, Rebecca Kadaga ameihoji Serikali sababu za kutumia nguvu kulizuia tamasha la Mbunge wa Kyaddondo, Robert Kyagulanyi.

Mbunge huyo licha ya kuwa mwanasiasa lakini pia ni mwanamuziki aliyejozolea mashabiki wengi nchini humo.

Spika alimuuliza Waziri Mkuu Dk Ruhakana Rugunda, kwamba ni nani aliyechukua jukumu Bunge kutoa uamuzi juu ya suala hilo.

Kadaga alisema hayo baada ya Walinzi wa Ulinzi nchini humo Jenerali Elly Tumwine kushindwa kuelezea sababu za kumzuia mbunge huyo kuendelea na tamasha lake.

“ Kyagulanyi atakuwa shahidi yangu, alipoamua kuingia Bungeni akiwa mwanamuziki nilizungumza naye na nikamuuliza atawezaje kufanya kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja Muziki na Siasa?’’alihoji Jenerali Tumwine

 



Chanzo: mwananchi.co.tz