Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Snoop Dogg na Master P walishtaki duka kubwa la Walmart

Snoop Dogg Na Master P Walishtaki Duka Kubwa La Walmart Snoop Dogg na Master P walishtaki duka kubwa la Walmart

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Rapa wa Marekani Snoop Dogg na Master P wanaishtaki kampuni ya maduka makubwa ya Walmart na kampuni ya kutengeneza vyakula kwa kuhujumu chapa yao ya nafaka.

Kesi iliyowasilishwa Jumanne inashutumu Walmart na Post Consumer Brands kwa kuficha masanduku ya Snoop Cereal na kusema kimakosa kuwa nafaka hiyo imeisha.

Wakili Benjamin Crump aliitaja hatua hiyo kama "kutozingatia wazi" biashara inayomilikiwa na watu weusi.Katika taarifa, kampuni zote mbili zinaonyesha mauzo ya chini ya bidhaa.

Walmart ilisema ina "historia dhabiti ya kusaidia wajasiriamali" na "mambo mengi huathiri mauzo ya bidhaa yoyote".

Wakati huo huo Post ilisema: "Tulisikitishwa vile vile kwamba mahitaji ya watumiaji hayakukidhi matarajio."Snoop Dogg na Master P walianzisha kampuni yao ya chakula, Broadus Foods, mwaka wa 2022.

Kulingana na tovuti yake, inazalisha nafaka za kiamsha kinywa, mchanganyiko wa pancake, sharubati ya maple na zaidi.

Kulingana na malalamiko hayo, yaliyonukuliwa na vyombo vya habari vya Marekani, Post ilijaribu "kuiondoa Broadus Foods nje ya soko" kwa sababu wasanii hao wa rapa walikataa kuuza kampuni hiyo kwa watengenezaji chakula.

Lakini walikubaliana kwa ushirikiano ambapo Post ingezalisha na kusambaza bidhaa kwa wauzaji wakubwa.

Bw Crump, ambaye ni mmoja wa mawakili mashuhuri wa haki za kiraia wa Marekani alichapisha video mtandaoni, akisema: "Hawangeweka nafaka mbele, waliificha nyuma ya ghala.

"Kesi hiyo inadai kuwa Walmart na Post Consumer Brands "zilihakikisha kwamba Snoop Cereal haitapatikana kwa watumiaji" au kwamba Broadus Foods "itaingiza gharama kubwa sana ambazo zingeondoa faida yoyote".

"Post kimsingi ilifanya kazi na Walmart kuhakikisha kuwa hakuna sanduku hata moja la Snoop Cereal litakaloonekana kwenye rafu za duka zilizo mbele"

Master P alichapisha video kwenye ukurasa wake wa Instagram ambayo inakusudia kuonyesha maduka kadhaa ya Walmart yakionekana kukosa bidhaa hiyo.

Katika onyesho hilo, wafanyikazi wasiojulikana wa Walmart katika maduka kadhaa wanaulizwa ikiwa wanauza nafaka, na wanapoingia katika mfumo wa Walmart wanasema bidhaa imeisha.

Kisha wanaonekana kugundua shehena ambazo hazijafunguliwa za Snoop Cereal kwenye chumba cha kuhifadhia.

Katika taarifa yake, Kampuni ya Post Consumer Brands pia ilisema "imefurahishwa na kushirikiana na Broadus Foods" na kusema ilifanya "uwekezaji mkubwa" katika biashara hiyo.

Walmart ilisema "itajibu inavyofaa mahakamani" mara tu itakapoona malalamishi kamili. .

Chanzo: Bbc